Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameanza kufanyia kazi Agizo la Rais Dr. John Magufuli la kufuatilia taratibu za ujenzi wa Barabara ya kutokea Makao Makuu ya BAKWATA hadi Biafra na tatizo la mfumo wa maji kwenye eneo la Kinondoni Shamba.
Mapema leo RC Makonda amefanya ziara ya ukaguzi na kubaini nyumba nyingi kwenye eneo hilo zimejengwa kwenye hifadhi ya barabara na baadhi ya watu tayari wamelipwa fidia ambapo amewataka wananchi kushirikiana na TARURA kuhakikisha ujenzi wa barabara unaanza Mara moja.
Aidha RC Makonda ameagiza TANESCO, DAWASCO na TTCL kushirikiana kwa karibu na TARURA kuondoa miundombinu yao ili kasi ya ujenzi ianze.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Kinondoni Bwana Leopold Runji amesema tayari wameanza utekelezaji wa maagizo waliyopatiwa na watahakikisha ujenzi unaenda kwa kasi na kukamilika kwa wakati.
Itakumbukwa kuwa tarehe 12 June,2018 Rais Dr. John Pombe Magufuli alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti na maendeleo ya ujenzi wa Makao Makuu ya BAKWATA ambapo wakati wa kuondoka alipata wasaha wa kuzungumza na Wananchi ambao waliwasilisha kwake ombi la ujenzi wa Barabara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa