Meli kubwa ya Jeshi la Jamhuri ya China yenye Hospitali ndani imewasili Leo ikiwa na Madaktari Bingwa 381, Vifaa na Madawa ya kutosha kwa ajili ya kuanza kwa zoezi la Upimaji na Matibabu Bure kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametembelea Meli hiyo na kujionea namna imesheheni Vifaa tiba vya Kisasa ambapo ndani yake vipo vyumba 8 vya Upasuaji, Vyumba vya ICU, Wodi za Wagonjwa, Vyumba vya Madaktari, Mitambo ya kisasa, Mahabara na Sehemu ya Wagonjwa kupumzika.
Meli hiyo ya kipekee ina Helicopter kwa ajili ya wagonjwa ambapo kwa Ulimwenguni Meli za Aina hiyo zipo Mbili pekee ambapo moja ni hii iliyokuja Tanzania na nyingine ipo Nchini Marekani.
RC MAKONDA amesema Meli hiyo ina mfumo maalumu wa Mawasiliano Kati ya Meli na Taifa la China pale inapotokea Ugonjwa umeshindikana.
Tayari Jopo la wataalamu 30 wameenda Hospital za Amana, Temeke, Mwananyamala na Ocean Road kwa ajili ya kukarabati na kufunga vifaa vipya kwa vile vitakavyobainika vilivyoharibika au Kufa.
Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma.
Amewasihi Wananchi wenye magonjwa yaliyoshindikana kwa muda mrefu kuchangamkia Fursa hii ya matibabu Bure chini ya Madaktari Bingwa kutoka China.
Kwa upande wake kiongozi Mkuu wa Meli hiyo Kamanda GUAN BAILIN amesema wamekuja na vifaa vya kutosha na madaktari waliobobea hivyo wananchi Wajitokeze kwa wingi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa