-Kamati ya Uchunguzi imekamilisha kazi na Ripoti kukabidhiwa Mamlaka za Juu
-Aipongeza Mamlaka ya Bandari kutekeleza Maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kwa kununua kifaa Cha kubaini wote watakaochepusha mafuta kutoka Bomba kuu
-Awataka wote waliojiunganishia mabomba kutoka Bomba kuu Kujisalimisha
Mhe Makalla akiongea na waandishi wa habari leo allipo zuru katika eneo la "Flow Meter" Bandari ya Dar es Salaam (TPA)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla ametembelea Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) leo Agosti 20, 2021 na kukuta utekelezwaji Mkubwa wa Maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Mkoa ya Ulinzi na Usalama (KUU) Ili kuboresha huduma zinazotolewa Bandarini hapo.
Akiwa Bandarini hapo Mhe. Makalla ameeleza kuwa Kamati ya Uchunguzi wa wizi wa Mafuta imekamilisha kazi na Ripoti kukabidhiwa Mamlaka za Juu.
Aidha, Mkuu wa Mkoa ametumia nafasi hiyo kuipongeza Mamlaka ya Bandari kwa kutekeleza Maagizo ya Kamati ya Mkoa ya Ulinzi na Usalama (KUU) iliyowataka kununua kifaa cha kubaini wezi wanaochepusha mafuta kutoka Bomba kuu ambapo alifanya ukaguzi wa kifaa hicho Ili kujionea ubora na ufanisi wa kifaa hicho.
Wakati huo huo Mhe. Makalla amewataka wale wote waliojiunganishia mabomba katika Bomba Kuu Kujisalimisha Mara moja.
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa amekagua Ukarabati na Ujenzi wa Barabara za kuingia na kutoka Bandari ambapo amekuta Ujenzi unaendelea na kumuagiza Mhandisi wa mradi huo kuukamilisha kwa viwango, kwa wakati na kuzingatia thamani ya fedha ,Value for money
Vilevile amekagua Gati namba Sifuri (0) ambapo amejionea maboresho ya kuongezwa kwa kina chake na upanuzi.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amewahakikishia watumiaji wote wa Bandari ya Dar es Salaam kuwa MWAROBAINI wa CHANGAMOTO zilizokuwa zinaikabiri Bandari hiyo umepatikana.
ReplyForward |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa