- Asema Maelekezo ya Rais Dkt Samia Suluhu kipaumbele ni wahanga kwanza soko likikamilika
-Awatoa hofu wafanyabishara asema Soko jipya litakuwa na uwezo wa kubeba wafanyabishara zaidi ya 4000 ukilinganisha na awali.
-Awahakikishia wafanyabishara Soko litakamilika Octoba, 2023 kwa viwango na Ubora zaidi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo ametembelea Soko la Kariakoo na kufanya mkutano wa hadhara na wafanyabishara wa Soko kubwa na dogo katika eneo la nje ya Soko hilo Ilala Jijini Dar es Salaam.
RC Makalla amesema WAHANGA wa Soko watapewa kipaumbele Soko likikamilika, watu waache upotoshwaji hakuna maombi mengine, waingie kwanza wenye Soko lao ambao walikuwepo toka mwanzo, na " hayo ni maelekezo ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan mara soko likikamilika wahanga ni namba moja" alisisitiza RC Makalla
Aidha RC Makalla amewatoa hofu wafanyabishara akisema awali soko hilo lilikuwa na uwezo wa kubeba wafanyabishara 2000 tu sasa likikamilika litaweza kubeba *wafanyabishara zaidi ya 4000 hivyo ni fursa pia kwa wafanyabishara wengine wakiwemo wamachinga.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amesema Ukarabati na Ujenzi wa Soko umefikia asilimia 52 mkandarasi anaenda na muda vizuri uwezekano wa kukamilisha mradi mapema ni mkubwa zaidi lakini ifikapo Octoba, 2023 Soko litakuwa limekamilika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa