- Ataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuongeza Kasi ili kufikia Asilimia 100.
- Aelekeza Viongozi kufanya ziara Mtaa kwa Mtaa ili kujirudhisha.
- Akaribisha Makampuni na Taasisi kujitolea kufadhili gharama za utengenezaji wa vibao na kuweka nembo zao ili kujitangaza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amepokea taarifa ya utekelezaji wa awamu ya pili ya zoezi la anuani za Makazi ikihusisha uwekaji wa alama za Vibao kwenye Nyumba, Barabara na Mitaa ambapo amesema Mpaka Sasa Mkoa umefikia Asilimia 56.
Akizungumza wakati wa kikao kazi Cha pamoja kilicholenga kutoa maelekezo ya kuwekea Mkazo Operesheni hiyo, RC Makalla amesema ni lazima Mkoa huo ufanye vizuri kwenye zoezi Hilo kwakuwa ndio uso wa Nchi.
Ili kufanikisha Zoezi hilo, RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha wanafanya vikao na Watendaji ngazi ya Kata na Mtaa ikiwa ni pamoja na kufanya ziara za ukaguzi.
Aidha RC Makalla Awataka Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kushirikiana na Wadau watakaokuwa tayari kujitangaza kupitia zoezi Hilo kwa kugharamia gharama za utengenezaji wa vibao au kuchangia Vifaa ili waweze kuweka nembo zao kwenye vibao.
Hata hivyo RC Makalla ameendelea kusisitiza kuwa maeneo yenye migogoro yasifikishiwe huduma hiyo huku akiwataka Wakandarasi wa utengenezaji wa vibao na nguzo kuongeza juhudi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa