-Awashukuru UNESCO WHO, FAO, na UNDP kuunga mkono Kampeni ya safisha pendezesha DSM
-Awataka wakazi wa DSM kuendelea kutunza fukwe na kutumia bahari kujipatia kipato (Uchumi wa Blue)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla mapema leo amefanya usafi katika fukwe za Cocobeach pamoja na mashirika ya Kimataifa UNESCO, WHO, FAO UNDP katika kuunga mkono Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM
CPA Makalla ameyashukuru mashirika ya Umoja wa mataifa kwa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mkoa katika Kampeni ya Usafi, uwepo wao wakiwa kama mashirika ya Kimataifa unatoa hamasa kwa Jamii kuona jambo la usafi sio la DSM tu linathamani pia Kimataifa.
Aidha CPA Makalla amesema yuko tayari kupokea Mchango au Ushauri kutoka katika mashirika hayo kwa lengo la kuongeza nguvu katika Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM, pia amewaalika kushiriki katika usafi wa pamoja wa mwisho wa mwezi huu katika Wilaya ya Kinondoni.
Vilevile CPA Makalla amewataka wakazi wa DSM kuendelea kutunza fukwe kwa kufanya usafi kwa lengo la kutunza mazingira kwa faida ya uhai wa viumbe hai vya baharini, kukuza uchumi (uchumi wa blue) pia Utalii
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa