- Asema hadi sasa tayari Madarasa 570 yamekamilika
- Amshukuru Rais Samia kwa uamuzi sahihi wa kuelekeza fedha zaidi ya Bilioni 15 DSM
- Changamoto za wanafunzi waliofaulu na kukosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya Madarasa sasa itakuwa historia
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo amezuru katika shule ya Sekondari Kambangwa Kinondoni- Dar es Salaam.
RC Makalla akiwa katika shule hiyo alikagua Ujenzi wa vyumba vya Madarasa ambavyo vimejengwa kutokana na fedha za Mapambano dhidi ya Uviko-19 zilizotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiongea na waandishi wa habari RC Makalla amesema zoezi la Ujenzi wa vyumba vya Madarasa katika Mkoa linaendelea vema tayari vyumba vya Madarasa 570 vimekamilika na vyumba 173 viko katika hatua ya ukamilishwaji.
RC Makalla amesema anaungana na wananchi hususani Wilaya ya Kinondoni Kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa busara tena kwa uwazi kuelekeza fedha hizo katika Mikoa, DSM ikiwa mojawapo ili kuboresha miundombinu ya Elimu.
"Ujenzi wa vyumba vya Madarasa DSM unaenda kumaliza tatizo lililokuwa linatokea ambapo wanafunzi waliokuwa waliofaulu lakini wanakosa nafasi kutokana na uhaba wa vyumba vya Madarasa" Alisema RC Makalla
Aidha RC Makalla amewapongeza Wilaya ya Kinondoni na Mkuu wa shule ya Sekondari Kambangwa kwa kusimamia vizuri Ujenzi wa vyumba vya Madarasa na kukamilisha kwa wakati
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa