- Awataka TANROAD na TARURA Kuzingatia mapendekezo ya Ushauri wa wabunge Na Madiwani.
- Akerwa na tabia ya baadhi ya Wataalamu wanaojifungia maofisini na kujiamulia Barabara za kutengeneza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA. Amos Makalla amewaelekeza TANROAD na TARURA kuhakikisha uchaguzi wa Barabara zilizopo kwenye Mpango wa kujengwa au kuboreshwa unazingatia vipaombele na matakwa ya Wananchi.
RC Makalla amekemea tabia ya baadhi ya Wataalamu kujifungia maofisini na kujiamulia Barabara za kutengeneza na kutozingatia maoni ya Madiwani, wenyeviti wa mitaa na Wananchi jambo linalopelekea Miradi ya Barabara kupelekwa kwenye maeneo yasiyokuwa na uhitaji Mkubwa.
Akizungumza wakati wa kikao Cha Bodi ya Barabara Mkoani humo, RC Makalla ameelekeza Maamuzi ya Vikao vya *Baraza la Madiwani kuzingatiwa.
Kutokana na changamoto ya Barabara Mkoani humo, kikao kimeshauri suala la uwepo wa *mfuko wa Barabara ambapo RC Makalla amepokea wazo Hilo na kuahidi kulifikisha Mamlaka za Juu.
Katika Kikao hicho kimepokea taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Barabara iliyowasilishwa na TANROAD, TARURA na DMDP pamoja na upokeaji taarifa ya mfumo kuweka utaratibu mzuri wa uendeshaji shughuli za Bodaboda ikiwemo Mpangilio wa Vituo, Ulinzi na Usalama na ukusanyaji mapato ulioandaliwa na Wataalamu kutoka Chuo kikuu Cha Dar es salaam
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa