- Ampongeza Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuimarisha Uhusiano.
-Ashukuru Balozi wa ujerumani na uongozi wa Humburg kwa kufadhili fedha zaidi bilioni 6.
- Awataka wananchi kuchangamkia fursa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amezindua Kiwanda Cha Kuchakata taka na kuzigeuza kuwa Mbolea halisi Cha Mabwepande kilichojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 6 ikiwa ni ufadhili wa Serikali ya Ujerumani na Tanzania kupitia ushirikiano baina ya Jiji la Dar es salaam na Jiji la Hamburg.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, RC Makalla amesema Kiwanda hicho kimekuja wakati muafaka ambao Bei ya mbolea imepanda Kutokana na Vita inayoendelea baina ya Urusi na Ukraine na kutoa wito kwa Wananchi kununua mbolea hiyo.
Aidha RC Makalla amesema uwezo wa Mkoa huo ni kuzalisha zaidi ya Tani 23 za taka kwa siku hivyo kupatikana kwa Kiwanda hicho itasaidia kuwa na uhakika wa mahala pa kuzipeleka.
RC Makalla ametoa wito kwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kusimamia Vizuri uendeshaji wa Kiwanda kwa kuhakikisha *uzalishaji wa malighafi unakuwa wa kutosha
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa