- Asema Mkutano huo kufanyika Jiji DSM kwa siku Saba na kuhudhuriwa na watu 300 kutoka Nchi 140 ambao ni wanachama wa Baraza la Michezo duniani
- Akiri kutoa ushirikiano kwa waandaaji hao mwanzo mwisho na kumuagiza RAS kwa kushirikiana na ujumbe huo kutengeneza Sekretarieti nzuri itakayobeba watu muhimu
- Aongeza kuwa Ugeni huo utakuwa na Manufaa makubwa katika Nchi
- Kwa upande wake Col Joseph Bakari ambaye ni Mkurugenzi wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani ameipongeza Dsm na Tanzania kwa Ujumla
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 28 Novemba 2022 akiwa Ofisini kwake ametangaza Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Mwezi Mei, 2024 Jijini Dar es Salaam kwa muda wa siku Saba na kuhudhuriwa na watu 300 kutoka Nchi 140 ambao ni wanachama wa Baraza la Michezo Duniani
RC Makalla amekiri kutoa ushirikiano kwa waandaaji wa Mkutano huo mwanzo mwisho na kumuagiza RAS kwa kushirikiana na waandaaji hao kutengeneza Sekretarieti nzuri itakayobeba watu muhimu katika kufanikisha Mkutano huo
Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kuwa Ugeni huo Mkubwa kutoka Nchi 140 Duniani utakuwa na Manufaa makubwa katika Nchi yetu ya Tanzania hususani Dar es Salaam kwani utajenga mahusiano, utamaduni, utakuza utalii wetu, kukuza uchumi na faida nyingine nyingi
Kwa upande wake Col. Joseph Bakari ambaye ni Mkurugenzi wa Baraza la Michezo ya Majeshi Duniani ameipongeza Dar es Salaam na Tanzania kwa Ujumla kwa kuwa mwenyeji wa Mkutano huo Mkubwa wa Muhula wa 79 hakika Tanzania inaenda kufunguka zaidi kimataifa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa