- Ampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuitangaza Tanzania.
- Awahamasisha Wananchi kuipendezesha Dar es Salaam ili kuvutia watalii Na wawekezaji.
- Amesema kwa Sasa mkoa wa Dar es Salaam unapendeza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameongoza Wananchi wa Wilaya ya Ilala kwenye zoezi la Usafi wa pamoja eneo la Buguruni ambapo amesema Filamu ya Royal Tour iliyozinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan imekuja wakati muafaka ambapo mazingira ya Dar es salaam ni safi na yanavutia Watalii na Wawekezaji.
Akizungumza wakati wa Usafi wa pamoja ikiwa ni mkakati wa Mkoa kufanya Usafi kila Jumamos ya mwisho wa Mwezi, RC Makalla amempongeza Rais Samia kwa kuitangaza anzania kimataifa jambo linalovutia Watalii.
Aidha RC Makalla amesema lengo Mkoa huo ni kufanya Kampeni ya Usafi kuwa endelevu ili kushika nafasi za juu kwenye majiji yanayoongoza kwa Usafi Barani Africa ambapo kupitia Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM imewezesha Jijia Dar es salaam kushika nafasi ya sita kwa Usafi Africa.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema Serikali kupitia TANROAD imeridhia ombi la Kiwanda Cha Azam Bakhresa kwa kuwaruhusu kupendezesha eneo la mbele la Kiwanda kwa kupanda bustani ya kisasa na kuweka minyororo ili kuzuia Ufanyaji biashara holela uliokuwa umeshamiri kwenye eneo Hilo.
Hata hivyo RC Makalla amepokea msaada wa Vifaa vya Usafi kutoka Wadau wa Usafi walioamua kumuunga mkono kwenye Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa