RC Makalla wa tatu Kushoto wakati alipozuru katika Soko la Kisasa Kibada Wilaya ya Kigamboni- Dar es Salaam mapema leo.
RC Makalla akikagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali maalum kwa ajili ya kutoa huduma za Afya kwa wagonjwa wenye kifua kikuu Sugu Kigamboni-DSM
- Ampongeza kwa bajeti 2022/23 imeenda kugusa wananchi wengi katika huduma Za jamii ikwemo Afya, Maji Na Elimu kwa kufuta ada kidato Cha tano Na sita.
- Asema Bajeti 2022/23 ni hat trick ni zaidi ya kuupiga mwingi
- Fedha Za miradi ya maendeleo zinatolewa kwa wakati na hakuna mradi umesimama
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa Bajeti kuu ya Serikali kwa Mwaka 2022/23 ambapo amesema Bajeti hiyo imegusa Maisha ya Wananchi wengi katika Jamii hususani sekta za Elimu Baada ya kutangaza kufuta ada ya kidato Cha tano na sita.
RC Makalla amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa Ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya Kifua Kikuu Kanda ya mashariki inayojengwa Vijibweni Wilayani Kigamboni ambapo kukamilika kwake itasaidia Wananchi wa ukanda huo.
Aidha RC Makalla amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya Shilingi Milioni 688 za Ujenzi huo ambao kwa Sasa umefika Asilimia 40 na unatajariwa kukamilika mwishoni mwa mwezi October mwaka huu.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema Hospital hiyo itakuwa na uwezo wa kupokea na kuhudumia Wagonjwa 80 kwa siku na itakuwa na Madaktari bingwa wa kutosha.
Wakati huohuo RC Makalla ametembelea Ujenzi wa Soko la kisasa la Kibada lililogharimu Shilingi Bilioni 6.3 ambalo Ujenzi wake upo Asilimia 99 kukamilika ambapo litaanza kutumika muda wowote kuanzia sasa.
Ili kuhakikisha Biashara zinafanyika, RC Makalla ameelekeza Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni kuweka Mazingira Bora ya kuchochea biashara ikiwa ni pamoja na Miundombinu ya Barabara za kuingia na kutoka.
Hata hivyo RC Makalla amesema kuwa Soko Hilo Lina uwezo wa kupokea Wafanyabiashara 1,000 ambapo amepongeza *ubunifu wa Ujenzi wa Vizimba na kabati za kuhifadhi mizigo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa