-Asema ni Kutokana na ongezeko la Biashara katika Jiji la Dar es Salaam
-Afafanua DSM imetajwa kuwa Mega City kutokana na Ongezeko kubwa la Idadi ya watu
-Wafanyabiashara wapokea Maelekezo kwa furaha, wapongeza ujenzi wa kisasa unaendelea Soko la Kariakoo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Agosti 9,2022 ametembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati na Ujenzi wa Soko la Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Akiongea na Wafanyabishara wa Kariakoo RC Makalla amesema Mhe Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kuanza mchakato wa Karikaoo kufanya Biashara masaa 24 kutona na Ongezeko kubwa la Biashara katika Jiji la Dar es Salaam ili kuwarahusishia wafanyabishara fursa zaidi za Kibiashara.
Aidha RC Makalla amebainisha kuwa Jiji la Dar es Salaam limetajwa kuwa Mega City kutokana na Ongezeko la Idadi ya watu kila kikicha ni dhahiri kuna umuhimu wa eneo la Kariakoo na mitaa yake ikaboreshwa kwa *kuweka mataa, na Camera ili biashara zifanyike masaa 24 hiyo itapanua fursa zaidi za Kibiashara ndani na Nje.
Vilevile RC Makalla ameridhishwa na maendeleo ya ukarabati na Ujenzi wa Soko la Kariakoo huku akimpongeza kujengwa kwa vizimba vya Kisasa, pia kuwepo kwa mifumo mizuri ya taadhari za majanga ya moto na mkandarasi yuko ndani ya muda
Kwa Upande wa Wananchi na Wafanyabishara katika Soko hilo wamefurahishwa na maamuzi mazuri ya Serikali ya Ujenzi na Ukarabati wa Soko hilo pia uamuzi wa *kuruhusu biashara kufanyika masaa 24 ni jambo jema sana kwa mslahi mapana ya wafanyabishara na Wananchi kwa ujumla likini pia ni fursa ya kukuza Uchumi wa DSM na Taifa.
Ifahamike kuwa ukarabati wa Soko la Kariakoo kupitia Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe Samia Suluhu Hassan tayari imehidhinisha Tsh Bilioni 28 kwa ajili ya kazi hiyo RC Makalla amemhakikishia Mkandarasi Pesa ipo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa