RC Makalla Kulia akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa Bi Rehema Madenge kushoto wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Miaka 59 ya Mungano katika Viwanja ya Zakhem-Temeke
- Asema Muungano wa Tanzania ni wa mfano duniani, haujawahi kuterereka Na chini ya Rais Dkt, Samia utaendelea kuimarika
- Aeleza mafanikio lukuki ya muungano ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo
- Asema Rais Samia amekusidia mwendokasi ifike mpaka Vikindu, fedha Bilioni 9 kujenga Hospitali Mbagala kuu
- Awataka Wananchi kuenzi Na kulinda muungano
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla leo ameongoza Wananchi wa Mkoa wa huo kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo ametoa wito kwa Wananchi kusimama na Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kuuenzi na kudumusha Muungano.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika Uwanja wa Zakhem Mbagala, RC Makalla amempongeza Rais Dkt, Samia kwa kuwa kielelezo kuzuri Cha Muungano ambapo amesema ndani ya Miaka 59 yapo Maendeleo na Mafanikio Makubwa yaliyofanyika.
Aidha RC Makalla ametumia maadhimisho hayo kumuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Temeke na Meya wa manispaa hiyo kuhakikisha ujenzi wa Stendi ya kisasa ya mabasi ya Kusini unafanyika ambapo pia amesema Rais Dkt, Samia ametoa kiasi Cha Shilingi bilioni 9 kwaajili ya ujenzi wa Kituo Cha Afya Mbagala Kuu.
Kuhusu suala la kero za Muungano, RC Makalla amempongeza Rais Dkt, Samia kwa kuendelea kuzishughulikia mpaka Sasa zimebaki kero nne pekee.
Hata hivyo RC Makalla amesema maadhimisho hayo kiomkoa yanaenda sambamba na Uzinduzi na uwekezaji wa mawe ya msingi kwenye Miradi mbalimbali ya Maendeleo yenye thamani ya Zaidi ya Shilingi bilioni 23 mpaka April 29.
Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano yameenda sambamba na kauli mbiu isemayo "Umoja na Mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu."
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa