- Asema fedha hizo zimesaidia kuondosha michango ya nyumba kwa nyumba Kwa Wazazi na walezi
- Ataka Vyumba vya Madarasa kukamilika kabla ya Disemba 30 mwaka huu.
- Amuhakikishia Rais Dkt. Samia hakuna Mwanafunzi yoyote atakaekosa Fursa ya kusoma DSM
- Asisitiza Ubora wa Majengo yanayojengwa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo ameendelea na ziara ya ukaguzi Maendeleo ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa Mkoa huo na Leo ilikuwa zamu ya Wilaya ya
Temeke ambapo ameelekeza Halmashauri hiyo kuhakikisha Madarasa yanakamilika kabla ya Disemba 30 mwaka huu.
RC Makalla amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi sahihi ya kutoa fedha ili kuhakikisha kila Mwanafunzi anasoma kwenye mazingira Bora na kuwaondolea Wazazi usumbufu wa michango Kama miaka ya nyuma.
Aidha RC Makalla ameshuhudia Ujenzi wa Madarasa ukiendelea vizuri ambapo Wilaya ya Temeke ilipokea Shilingi Bilioni 4.1 kwaajili ya Ujenzi wa Madarasa 207 ikiwemo ya Gorofa na Mtawanyiko ambapo mpaka Sasa Madarasa 97 yapo kwenye ngazi ya Ujenzi wa Msingi, 32 ukuta, 67 Yanaezekwa na 11 Ujenzi unaanza kesho Baada ya kupatikana kwa maeneo.
RC Makalla pia amepokea taarifa ya Wilaya juu ya idadi ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo mwezi January mwakani ambapo Kwa Shule za Awali wanaotarajiwa ni wanafunzi 6,343, Msingi wanafunzi 26,000 na Sekondari 23,000.
Ifahamike kuwa Mkoa wa Dar es salaam ulipokea zaidi ya Shilingi Bilioni 12.3 kwaajili ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa kwaajili ya wanafunzi wa Shule za Awali, Msingi na Sekondari ambapo pia amesisitiza Ubora wa Majengo yatakayojengwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa