- Amepongeza Rais Dkt. Samia kutoa fedha bilioni 12 kujenga vyumba vya madarsa kuhakikisha kila Mwanafunzi anasoma.- Asema hakuna Mwanafunzi kuanzia Shule ya Awali, Msingi na Sekondari atakaekosa nafasi ya masomo
- Wazazi watakiwa kusimamia watoto wao waende Shule.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema hakuna Mwanafunzi kuanzia Shule ya Awali, Msingi Wala Sekondari Mkoani humo atakaeshindwa kwenda Shule kwa kigezo Cha uhaba wa Madarasa au Madawati Baada ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa Zaidi ya Shilingi Bilioni 12.3 za Ujenzi wa Madarasa.
RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara ya ukaguzi wa Maendeleo ya Ujenzi wa Madarasa Kwenye Shule ya Sekondari Misitu, Kerezange na Liwiti Wilaya ya Ilala ambapo ameshuhudia Ujenzi wa Madarasa yakiwa kwenye hatua nzuri.
Katika ziara hiyo, RC Makalla amepokea taarifa ya mwenendo wa Ujenzi kwa Wilaya ya Ilala ambapo jumla ya Shilingi Bilioni 6.2 zilitolewa kwaajili ya Madarasa 310 ya magorofa na Mtawanyiko kwenye Shule 34.
Ili kuhakikisha dhamira njema ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatimia, RC Makalla ameelekeza watendaji wote kuhakikisha Ajenda ya ukamilishaji wa Madarasa inapewa kipaombele ili kabla ya Mwezi January Madarasa yawe tayari na wanafunzi wasome.
Kwa mujibu wa Halmashauri ya Ilala makadirio ya wanafunzi watakaoanza masomo January mwakani kwa *Shule za Awali ni 5,700, Msingi 25,400 na kidato Cha kwanza 30,500.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa