- Hali ya usalama ni shwari, watuhumiwa 86 wa matukio panya road wamefikishwa mahakamani.
- Awahakikishia wananchi usalama, Jeshi la polisi Na vikundi vya ulinzi shirikishi wapo macho muda wote.
- Apongeza Jeshi la polisi, viongozi wa mitaa Na ulinzi shirikishi kwa kazi Nzuri.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Operesheni ya kukamata Panya road imefanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 86 na kuwafikisha Mahakamani kwaajili ya hatua za kisheria
RC Makalla amesema hayo wakati wa kikao Cha kupokea taarifa ya Operesheni ya kukamata Panya road ambapo Operesheni hiyo imefanikiwa kakamata Vitu vilivyokuwa vimeibiwa ikiwemo Runinga 13 na Simu 8 za mkononi.
Aidha RC Makalla amepongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya ambapo amesema kwa Sasa Mkoa upo Shwari hivyo hakuna sababu yoyote ya Wananchi kuwa na wasiwasi.
Hata hivyo RC Makalla amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Simon Sirro kwa uamuzi wake wa kutoa Afisa Polisi kwenye Kila Kata ya Mkoa huo ambapo ameelekeza agenda ya Ulinzi na usalama ipewe kipaombele kuanzia ngazi ya Mtaa,Kata mpaka Wilaya.
Pamoja na hayo RC Makalla amekemea tabia ya baadhi ya Wananchi kutumia mitandao ya kijamii kusambaza video za zamani jambo linaloweza kuleta taharuki kwa Wananchi.
Kutokana na kufanikiwa kwa Operesheni hiyo, RC Makalla amesema zoezi Hilo ni endelevu na amewaonya watu Wanaonunua Mali za Wizi ambapo amesema msako wa kuwakamata wanunuzi inaendelea.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam, Jumanne Muliro amesema Jeshi Hilo lipo macho kuhakikisha Linalinda usalama wa Raia na Mali zao
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa