- Atoa Wiki Moja kwa NEMC na TBS kuweka ratiba ya kutoa elimu kwa Wananchi Wilaya zote za DSM.
- Aonya Bar na Kumbi za starehe zinazopiga mziki mkubwa na kusababisha kero kwa Wananchi
- Aseme kikao Cha leo kimetanguliwa Na kikao Cha Vongozi wa Dini Kuhusiana na kero ya kelele nyumba Za ibada kwenye makazi.
- Ataka Sheria, Kanuni na taratibu za NEMC kufuatwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla ametangaza Kuanza kwa operesheni kabambe ya kukamata wazalishaji na Watumiaji wa Mifuko ya plastic iliyokatazwa kuanzia Mei Mosi ambapo amewataka Wananchi kuanza kuchukuwa tahadhari.
RC Makalla ameelekeza Baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC kwa kushirikiana na TBS kuweka ratiba ya Siku za kutoa elimu kwenye Wilaya zote za Mkoa huo kabla ya Kuanza kwa operesheni hiyo Ili kujenga uelewa.
Hatua hiyo imekuja baada ya matumizi ya mifuko ya plastic iliyokatazwa Kuanza kurudi upya Licha ya Serikali kupiga marufuku.
Akizungumzia wakati wa mkutano wa udhibiti mifuko ya plastic, Kelele za mziki na mitetemo, RC Makalla pia amewataka Wamiliki wa Bar na Kumbi za starehe na Vyombo vya mziki kufuata na kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo ya Baraza la uhifadhi na usimamizi wa mazingira NEMC ili kuepusha kero ya Kelele za mziki kwa Wananchi.
Aidha RC Makalla amesema kumekuwa na malalamiko Makubwa ya uvunjifu wa Sheria kufuatia ongezeko la Bar na Kumbi Za starehe kwenye makazi ya watu ikiwa ni pamoja na upigaji mziki usiku mzima na kuathiri Wananchi.
Katika mkutano huo uliohusisha Viongozi wa mitaa, Masoko na wadau wa mazingira, RC Makalla ameelekeza Viongozi wa Serikali za mitaa kuchukuwa hatua ikiwa ni pamoja na kudhibiti utoaji vibali vya ujenzi kiholela.
Kwa mujibu wa sheria na Kanuni za NEMC makosa na adhabu kwa wanaokiuka Sheria ya kupiga mziki kwenye makazi ya watu ni faini ya shilingi milioni 2 mpaka milioni 10, kifungo Cha Miaka miwili jela au vyote kwa pamoja na Sheria inaruhisu upigaji mziki kuanzia Saa 12 asubuh mpaka Saa nne usiku kwa kiwango kilichoruhusiwa na kwa bar zinazokesha nao wamepewa taratibu za kufuata Ili kupewa kibali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa