Mhe Amos Makalla akiongea na Machinga mtaa wa Msimbazi Kariakoo Mapema leo.
- Asema Kufanya biashara holela barabarani ni kukiuka Sheria na haki za watembea kwa miguu
- Amtaka Mkuu wa Wilaya ya Ilala kukaa na uongozi wa Machinga Kariakoo Septemba 13, 2021
- Asisitiza anawajibu wa kusimamia Sheria na Usalama wa wananchi wa Dar es Salaam
- Asema wamachinga ni watu muhimu katika nchi hii lakini ni vizuri kufuata utaratibu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla mapema leo Septemba 9,2021 amezuru eneo la msimbazi karibu na Jengo la Club ya Simba Kariakoo Ilala, Jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika eneo hilo Mhe Makalla alipata wasaa wa kutembea kwa miguu katika eno hilo kujionea namna wafanyabiashara wadogo walivyopanga biashara zao katika miundombinu ya barabara ya DART na kuwaathiri watembea kwa miguu kupata ajali wengine kupoteza maisha.
Mhe Makalla akiongea na hadhara iliyokusanyika kumsikiliza ametoa tamko kuwa kuanzia sasa njia za watembea kwa miguu na "road reserve" ni lazima ziwe wazi katika Mkoa wa Dar es Salaam kufanya biashara holela barabarani ni kukiuka sheria na haki za watembea kwa miguu.
" Ni vema kila mwananchi kuheshimu sheria na haki ya mwingine na mimi Mkuu wa Mkoa moja ya jukumu langu ni kusimamia sheria na haki za wananchi " Alisema *Mhe Makalla*
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa amesma biashara holela barabarani katika eneo la Kariokoo zinasababisha ajali na watu kupoteza maisha jana tu kuna watu wamegongwa na mwendokasi na wengine kupoteza maisha, nitoe pole kwa familia lakini hii hali sasa ifike mwisho.
Aidha amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala na timu yake Jumatatu Septemba 13, 2021 kukaa na uongozi wa Machinga Kariakoo na kuja na mpango wa kuwaondoa machinga katika miundombinu ya barabara ya DART Msimbazi pasipo kuathiri biashara zao ikiwezekana kubainisha sehemu ya kuwapeleka au kuwa na siku maalum za kufunga barabara fulani kuruhusu machinga kufanya biashara.
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan inawapenda wafanyabiashara wadogo hivyo katika Mkoa wa Dar es Salaam hakuna machinga atakayekosa sehemu ya kufanya biashara awataka kufuata utaratibu.
Kiongozi wa Machinga Kariakoo Ndg Lusinde amekiri kuwepo kwa biashara holela yeye na viongozi wenzake wako tayari kukaa na uongozi kwa wa Wilaya ili kuipatia ufumbuzi changamoto hiyo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa