- Acheza namba '8' timu ya viongozi wa dini dhidi ya wachambuzi wa habari za michezo
- Asema yeye ni kiongozi lazima awe mstari wa mbele, anachokifanya anamaanisha
- Asisitiza watu kufanya mazoezi na kuchanja chanjo ya UVIKO-19
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Septemba mosi ameonyesha ubora wake katika kusakata kabumbu akiwa kiungo hatari wa timu ya Viongozi wa Dini dhidi ya wachambuzi wa habari za michezo* mechi ambayo imechezwa katika uwanja wa Azam Chamazi na kupelekea kutoka sare ya bao tatu kwa tatu ( 3 - 3).
Akiongea uwanjani hapo Mkuu wa Mkoa amesema michezo ni afya, michezo ni ajira mechi ya leo imekuwa nzuri na hao tulio cheza nao leo tunataka mtanange urudiwe tena.
Aidha akafafanua lengo la mtanange huo ni kuhamasisha wananchi hususani wa Mkoa wa Dar es Salaam kutumia fursa ya kuchanja chanjo ya UVIKO-19.
" Leo mchezo umekuwa na mafanikio makubwa watu wengi wamejitokeza kuchanja toka saa tisa na lengo la mtanange huu ni kuhamasisha jamii kutumia fursa hii ya chanjo, niendelee kutoa rai watu wachanje kama Rais wetu *Mhe Samia Suluhu Hassan* amechanja na mimi na viongozi wenzangu Mkoani tumechanja unasubiri nini" Alisema Mhe Makalla
Aidha Mhe Makalla abainisha kuwa yeye ni muumini wa mazoezi na ndio maana amecheza dakika zote bila kuchoka, hivyo ukiwa kiongozi unapaswa kuwa mstari wa mbele na siku zote kile anachokiongea anamaanisha na leo mmekuwa mashuhuda.
Mtanange huo ulikuwa wa kuvutia huko ukishuhudiwa na waziri wa Afya Mhe Dorothy Gwajima na Waziri wa Habari Mhe Innocent Bashugwa na watu wengine maarufu.
Mhe Amos Makalla anaendelea kuhimiza wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam kuendelea kufanya mazoezi kwa kuwa ni Afua mojawapo ya Kupambana na ugonjwa wa UVIKO-19 na magonjwa mengine nyemelezi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa