-Atangaza Kukamatwa Watuhumiwa wengi Kwenye Operesheni Matukio ya Tabata, Kawe na Mizimuni
-Asema Watuhumiwa Wengi ni waliotoka Magerezani na Kumaliza Vifungo
-Awahakikishia Wananchi Ulinzi Umeimarishwa Askari 300 Wameongezwa
- Ataka Ulinzi Shirikishi kila Mtaa, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi
-Wananchi waombwa taarifa za Kusaidia Operesheni na Sio Upotoshwaji na Kuzusha hofu
RC Makalla amesema Mazazi mwenye mtoto Panya Road kuanzia leo Septemba 15, 2022 asipomuona nyumbani asihangaike akamtafute mwanae Kituo cha Polisi au Hospitali
RC Makalla ameyasema haya mapema leo katika Mkutano wa hadhara na Wananchi wa Kata ya Zingiziwa Chanika Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam.
Mhe Makalla ametangaza Kukamatwa kwa Watuhumiwa Wengi *kwenye Operesheni katika Matukio ya Tabata, Kawe na Mizumuni ambapo amesema Watuhumiwa wengi ni wale waliotoka magerezani na kumaliza vifungo hivyo ametoa rai na ana imani na mahakama kuwa itatenda haki wale ambao makosa yao yana rudia rudia hukumu yao iwe kali zaidi
Aidha RC Makalla amewahakikishia wananchi wa DSM kuimarika kwa Ulinzi Askari 300 Wameongezwa kushughulika na Panya Road wananchi wasiwe na hofu waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo
Vilevile Mhe Makalla ametaka Ulinzi Shirikishi kila Mtaa kwa kushirikiana na Polisi na tayari Wakuu wa Wilaya wote DSM wanamaelekezo ya kusimamia jambo hilo kwa weledi mkubwa.
Sambamba na hilo RC Makalla ametoa Rai kwa wananchi kutoa taarifa za Kusaidia Operesheni na Sio Upotoshwaji na Kuzusha hofu huku akiwataka wananchi kutumia mitandao ya kijamii vizuri
" Tusitumie mitandao kutengeneza hofu na Wananchi wetu kukaa kwa wasiwasi, Taarifa ni muhimu sana lakini ziwe taarifa zenye uhakika " Amesisitiza RC Makalla
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa