- Ampongeza *Rais Dkt. Samia kufanikisha mradi kutoka asilimia 12 aliyoikuta mpaka Sasa mradi umefikia asilimia 82.
- Ataka mradi kukamilika na kukabidhiwa Mwishoni mwa mwezi machi mwaka huu.
- Aelekeza Wanaofanya biashara kwenye eneo lililokatazwa Mbagala kuondolewa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amemuelekeza Mkandarasi wa kampuni ya Sino Hydro anaejenga Barabara ya mwendokasi BRT kutoka katikati ya mji kuelekea
Mbagala kuhakikisha ifikapo mwishoni mwa mwezi machi Mwaka huu mradi uwe umekamilika.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Barabara za BRT unaohusisha ujenzi wa Barabara ya Km 20.3, Madaraja ya Juu na Vituo 21 vya kushusha na kupakia abiria.
Aidha RC Makalla amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuendeleza mradi huo kutoka asilimia 12 mpaka Sasa ambapo Mradi umefikia asilimia 82 na kumpongeza Mkandarasi kwa jitiada kubwa anazoonyesha.
Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza TANROAD, TRC, TANESCO na DAWASA kuweka utaratibu mzuri wa kufanya kazi kwa kushirikiana ikiwa ni pamoja na kuondoa Miundombinu Yao kwa wakati Ili Kumuwezesha Mkandarasi kufanya kazi yake.
Katika hatua nyingine RC Makalla amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Katibu tawala na Mkurugenzi kuhakikisha Wafanyabiashara wanaofanya Biashara kwenye maeneo yaliyokatazwa ikiwemo Mbagala Rangitatu kuwaondoa na kuwapeleka kwenye maeneo walipopangiwa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa