- Ampongeza *Rais Samia kwa kutoa pesa ambazo zimejenga vyumba vya Madarasa 743
- Awataka Watendaji na Viongozi DSM kuendelea kutoa ushirikiano na ofisi yake kama ilivyofanyika katika Kampeni ya kuwapanga vizuri wamachinga
-Apongeza Jeshi la polisi kwa kuendelea kusimamia Ulinzi na Usalama katika Mkoa
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla wakati anafungua *Kikao cha Bodi ya Ushauri ya Mkoa (DCC)* katika Ukumbi wa Mikutano Arnatoglo-Ilala Jijini Dar es Salaam.
RC Makalla amesema Mkoa umeendelea kutekeleza Mipango mbalimbali ya Serikali ikiwemo kutekeleza Mipango na bajeti ya Mkoa ya mwaka 2021/2022
Katika kutekeleza Mipango hiyo RC Makalla amesema Ofisi yake ilitoa maelekezo nane kwa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa DSM miongoni mwa maelekezo hayo ni Ukusanyaji wa mapato, Usimamizi mzuri wa miradi ya maendeleo na Kusikiliza kero za wananchi
Aidha RC Makalla amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa busara yake ya kutafuta mkopo wenye mashariti nafuu, pesa ambazo akazigawa kwa uwazi nchi nzima ambapo DSM pekee yake imepata zaidi ya Bilioni 15 zote zimeelekezwa kujenga vyumba vya Madarasa 743 ambavyo kwa sehemu kubwa vinaenda kuondoa Changamoto za Upungufu wa Madarasa kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa amewataka Watendaji na Viongozi DSM kuendelea kutoa ushirikiano ili Mkoa ufanye Vizuri zaidi kama ilivyofanyika katika Kampeni ya kuwapanga vizuri wamachinga, Safisha Pendezesha Dar es Salaam, kinacho hitajika sasa ni kuendeleza.
Pamoja na hayo RC Makalla amelipongeza Jeshi la polisi kwa kusimamia vema Ulinzi na Usalama katika Mkoa na amewahakikishia Wakazi wa Mkoa wa DSM kuwa ni Salaama wananchi wakasherekee vizuri Sikukuu ya mwaka mpya 2022.
Kwa upande wa mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam Bi Kate Kamba amesema Mkoa wa DSM una kila sababu ya Kumshukuru Rais Mhe Samia Suluhu kwa Kutoa pesa zinazogharimia miradi mikubwa inayotekelezwa ikiwemo ya Barabara, Vyumba vya Madarasa na mingine mingi, ametoa RAI wananchi kuunga Mkono Juhudi zinazofanywa na Rais
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa