- Ampongeza kwa uamuzi wa kuhakikisha maeneo ya pembezoni yanapata huduma ya maji.
- Awamwagia sifa DAWASA kwa utendaji mzuri.
- Awaonya Wananchi wanaoiba mita Za maji.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Miradi yote ya Maji inayotekelezwa pembezoni Mwa Mji ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma ya Maji safi inawafikia Wananchi wote ambapo amewapongeza DAWASA kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya.
RC Makalla ameyasema hayo wakati wa ziara ya kukagua Mradi Mkubwa wa usambazaji wa Maji kutoka Tank la maji Kisarawe kuelekea Pugu, Gongolamboto na Maeneo jirani uliogharimu Shilingi bilioni 7.3 ambapo tank la Pugu lina uwezo wa kupokea Lita Milioni mbili za maji.
Katika Ziara hiyo RC Makalla amepokea shukrani na shuhuda za Wakazi wa Pugu ambao Wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwafikishia huduma ya maji majumbani na kutatua Kilio Cha muda mrefu Cha ukosefu wa Maji kilichokuwa kikiwakabili.
Aidha RC Makalla amewapongeza DAWASA kwa utekelezaji wa Miradi kwa kutumia fedha za ndani ambapo pia amesifu ubunifu wa kuwaunganiahia Wananchi maji kwa mkopo.
Hata hivyo RC Makalla amekemea Wizi wa Miundombinu ikiwemo Mabomba na Mita za Maji jambo linalorudisha nyuma Nia Njema ya Serikali kwa Wananchi wake.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amewasilisha kwa RC Makalla ombi la ziara ya siku tano ya kutembelea na kujionea miradi mikubwa ya Maji inayotekelezwa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo kukamilika kwake kutasaidia upatikanaji wa huduma maji kila kona ya Jiji Hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa