Baadhi ya wamachinga wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Mkoa CPA Amos Makalla
Mwenyekiti wa Mchinga DSM Ndg Yusuph Namoto akiongea wakati wa kongamano hilo katika ukumbi wa PTA Sabasaba Jijini Dar es salaam
- Machinga DSM wamtunuku Tuzo Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uongozi mahiri na kuwajali machinga.
- Atoa maagizo 6 kwa Wakuu Wilaya kuhusiana Na kuboresha masoko Na utatuzi wa kero Za machinga.
Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam na mlezi wa Machinga CPA, Amos Makalla akizungumza na maelfu ya Machinga kwenye Kongamano lililofanyika Ukumbi wa PTA Sabasaba amewahakikishia Wafanyabiashara hao kuwa Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Itaendelea kulea na kulinda kundi Hilo ikiwa ni pamoja na kuboresha mazingira yao.
Akizungumza wakati wa Kongamano hilo RC Makalla amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na maafisa Biashara kuhakikisha Kila Soko linakuwa na Maji na vyoo na kuwataka kufanyika vikao vya mara kwa mara Ili kujua changamoto zao.
Aidha RC Makalla amewaelekeza LATRA kuhakikisha wanaweka route za Daladala kwenye Kila soko Ili kuchagiza na kuchochea Biashara.
RC Makalla pia ametumia Kongamano hilo kuelekeza Halmashauri zote kuhakikisha ujenzi wowote wa masoko unashirikisha pia mawazo ya Viongozi wa Machinga wa eneo husika ili kuepuka tatizo la ujenzi wa masoko ambayo sio rafiki kwa Biashara
Kuhusu hatma ya Wafanyabiashara Soko la Kariakoo walioondolewa kupisha ujenzi, RC Makalla amesema Soko likikamilika kipaombele Cha kwanza kitakuwa kwa wazawa waliokuwepo na kueleza kuwa mwelekeo baada ya Soko kukamilika ni Biashara saa 24.
Pamoja na hayo RC Makalla amewaelekeza Wakurugenzi kuhakikisha kipaombele Cha Mikopo ya asilimia 10 inatolewa kwa wanaofanya shughuli za Machinga.
Hata hivyo RC Makalla ametoa Wito kwa taasisi za Bank kuwafikia Machinga na kuendelea kutoa mikopo rafiki kwa Wafanyabiashara
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa