- Ashuhudia kushuka kwa kina Cha maji Ruvu juu na Chini.
- Uwezo wa uzalishaji wa maji umeshuka kutoka Lita Milioni 466 mpaka Lita Milioni 300.
- Awataka Wananchi Kumuomba Mungu mvua zinyeshe na kutumia Vizuri kiasi Cha maji yaliyopo.
- Aagiza Kukamilika kwa visima vya Maji Kigamboni kuongeza Upatikanaji wa maji Kigamboni na katikati ya mji.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema tatizo la mgao wa maji jijini humo kwa Sasa ni matokeo ya kiangazi kilichosababishwa na kukosekana kwa mvua za Vuli jambo lililopelekea kushuka kwa kina Cha maji kwenye vyanzo vya Maji Ruvu juu na Chini.
RC Makalla amesema hayo wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na usalama kwenye vyanzo vya Maji Ruvu juu na Chini ambapo ameshuhudia kina Cha maji kikiwa kimeshuka kutoka uwezo wa kuzalisha Lita Milioni 466 mpaka Lita Milioni 300 sawa na Asilimia 64.
Kutokana na Changamoto hiyo RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi kutumia Vizuri kiasi Cha maji yanayopatikana na kufanya Maombi ili mvua za Vuli zinyeshe.
Aidha RC Makalla amesema Kamati za Ulinzi na usalama Mikoa ya Dar es salaam, Pwani na Morogoro zilishatekeleza wajibi wa kudhibiti uchepushaji wa maji hivyo uhaba wa maji hauhusiani na Uzembe wa Aina yoyote.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema kukamilika kwa Visima vya Maji Kigamboni mwishoni mwa mwezi huu itasaidia Upatikanaji wa Lita Milioni 70 ambazo zitasaidia kupunguza makali kwa Wakazi wa Kigamboni na maeneo ya katikati ya mji.
Itakumbukwa Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania TMA ilishatoa taadhari ya uwepo wa kiangazi Kutokana na kuchelewa kwa mvua za Vuli jambo lililopelekea kushuka kwa kina Cha maji kwenye vyanzo vya Maji Ruvu juu na Chini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa