Mhe Amos Makalla akitoa Maelekezo akiwa Jimbo la Kibamba wakati wa muendelezo wa ziara yake ya Jimbo kwa Jimbo kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
-Asema anatembea na Clinic Inayotembea
-Asema KERO kubwa ya MAJI kibamba kuwa historia
-Ataka Ushirikiano Kati ya wananchi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama
-Akemea Biashara holela Dar es Salaam
-Asisitiza ushirikishwaji wa Viongozi Ngazi ya Mtaa kabla ya utekelezaji wa Mradi
Hayo yamesemwa Leo tarehe 31 Agosti, 2021 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla katika muendelezo wa kusikiliza KERO za wananchi katikaJimbo la Kibamba Wilaya ya Ubungo.
*Mhe. Makalla* amesema kuwa ameamua kuwafuata wananchi ili kuwasikiliza na kutatua changamoto walizonazo ambapo anatembea kila Jimbo na "Clinic Inayotembea" yaani akiwa ameongozana na Wataalamu wote wanaohusika." Ofisi yote Imehama ili kuwafuata na kuwahudumia wananchi" Alisema Mhe. Makalla
Akiwa katika Jimbo Hilo Mhe. Mkuu wa Mkoa amepokea KERO mbalimbali ambazo ni pamoja na Kero ya Urasimishaji, ajari nyingi kutokea katika Barabara ya Kimara mpaka Kibaha, tozo kubwa katika Parking za malori, Vituo vya kuuzia mafuta kuondolewa, Migogoro ya Ardhi, na wananchi kuchukuliwa maeneo yao bila fidia.
Kuhusu KERO kubwa inayolikabili Jimbo la Kibamba ya MAJI Mhe. Makalla amesema kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imetenga kiasi cha shilingi billioni 5.4 kwa ajili ya Ujenzi wa Tanki la Kubwa la Mshikamano linaloenda kumaliza tatizo la maji katika Jimbo hilo na litakamilika Juni 2022.
Aidha miradi midogo midogo inaendelea kujengwa na DAWASA ili kuendelea kupunguza shida ya maji.
Wakati huo huo Mhe. Makalla ametaka kuwepo kwa ushirikiano kati ya Wananchi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambapo amesisitiza kuwa ili wananchi waishi kwa Amani na Utulivu ni vema kuwafichua wahalifu wote waliopo miongoni mwetu.
Mhe. Mkuu wa Mkoa amekemea pia suala la Biashara holela na kusema hazitakiwa katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema anashangaa kuona utaratibu mbovu wa baadhi ya wafanyabiashara kuweka Biashara kila sehemu, kuvamia kila upenyo na wengine kupika chakula sehemu hatarishi bila kujali Usalama wao, amesisitiza kuwa hakuna mfanyabiashara atakayekosa sehemu ya kufanyia biashara Dar es Salaam.
" Tunawafuata wananchi popote walipo ili tuwahudumie na huu ndio Msukumo wa Mhe. Rais". Alisisitiza Mkuu wa Mkoa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa