- Awataka wananchi kuanza matibabu kwa wale waliogundulika Na magonjwa yasiyoambukiza
- Awashukuru Clouds Media group, Madaktari Na wadau wengine waliofanikisha kampeni ya Afya chek.
- Aelekeza Uwepo wa Hospitali tembezi Kwa madaktari bingwa katika kila wilaya.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo Juni 13 amehitimisha zoezi la siku kumi za upimaji Afya Bure ambapo mpaka kufikia siku ya Jana Juni 12 zaidi ya Wananchi 7,030 walihudumiwa na madaktari bingwa na wabobezi kutoka Hospital kubwa za Mkoa huo.
Akihitimisha zoezi Hilo RC Makalla amesema zoezi Hilo limekuwa na mafanikio makubwa ambapo Kati ya Wananchi 7,030 waliohudumiwa, Wananchi 1,522 walipima Shinikizo la Damu, 247 Kisukari, 808 walipimwa tatizo la moyo, uchangiaji wa Damu unit 203, kipimo Cha ultrasound 1,726 , 189 tezi dume, 949 walipata Chanjo ya COVID-19, 601 walipima Saratani ya shingo ya kizazi, 1,369 walipima tatizo la meno na macho Wananchi 1,673.
Kutokana na mwamko kuwa mkubwa, RC Makalla amemuelekeza Katibu Tawala wa Mkoa huo kuanzisha huduma ya Hospital inayotembea Mobile hospital kwa kutumia gari maalumu litakalokuwa limesheheni madaktari bingwa.
Aidha RC Makalla ametumia zoezi Hilo kutoa wito kwa Wananchi kujiwekea utaratibu wa Upimaji Afya Mara kwa mara Kutokana na takwimu kuonyesha Wananchi wengi waliogundulika kuwa na matatizo ya Afya hawakuwa na wakitambua.
Hata hivyo RC Makalla amewasisitiza Wananchi kufanya mazoezi ili kujiepusha na hatari ya kupata magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo Kisukari, Shinikizo la Damu, Saratani na magonjwa mengineyo.
Pamoja na hayo RC Makalla amewashukuru Wadau waliofanikisha zoezi Hilo wakiwemo Clouds Media group kupitia kipindi Cha Afya Check ambao ndio waratibu wa zoezi Hilo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa