.
- Asema kazi ya kurejebisha Miundombinu iliyoungua itafanyika usiku na mchana.
- Awahakikishia Wafanyabiashara hakuna atakaehamishwa.
- Asisitiza Masoko kuwa na Fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO.
- Aonya tabia ya Mamalishe kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema chanzo Cha Moto uliopelekea kuteketea kwa Soko la Veterinary lililopo TAZARA Wilaya ya Temeke ilitokana na Hitilafu ya umeme.
RC Makalla amesema hayo alipotembelea Soko Hilo kujionea uharibifu wa Mali zilizoteketea moto ambapo amesema taarifa za awali zinaonyesha Moto huo umeathiri takribani vibanda 453
Aidha RC Makalla amesema Serikali inafanya taratibu za haraka kuhakikisha kazi ya kurejesha Miundombinu iliyoharibika inafanyika usiku na mchana ili Wafanyabiashara warudi kuendelea na Biashara Kama awali ambapo ameahidi hakuna mfanyabiashara atakaeondolewa.
Hata hivyo RC Makalla ametoa pole kwa Wafanyabiashara walioathiriwa na Moto huo na kuwataka kuwa watulivu wakati Serikali yao inaendelea kutatua changamoto hiyo.
Kutokana na matukio ya Moto kujirudia Mara kwa Mara, RC Makalla ameendelea kutoa wito kwa Viongozi wa masoko kuhakikisha kila soko linakuwa na fundi umeme anaetambuliwa na TANESCO,Halmashauri kuweka Vifaa vya kudhibiti moto kwenye Kila soko, Wafanyabiashara kuacha tabia ya kuhinjika maharage jioni ili asubuhi wakute yameiva huku akisisitiza Masoko kuwa na Ulinzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa