- Asema kuhusu shule kuuzwa ni maombi yaliyowasilishwa ili yajadiliwe na bodi ya shule, kata, wilaya, mkoa mpaka Taifa.
- Kuhusu mikopo ameagiza CAG afanye ukaguzi maalumu ili kujua mwenendo wa utoaji mikopo Na marejesho.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amemaliza Hali ya *taharuki juu ya uvumi wa taarifa zilizodaiwa kuwa eneo la Shule ya Sekondari Kurasini linauzwa kwa Mwekezaji ambapo amethibitisha kuwa eneo Hilo haliuzwi.
RC Makalla amesema ni kweli kuwa Mwekezaji alituma *Maombi ya kupatiwa eneo* Hilo la Shule na kuahidi kujenga shule nyingine eneo la Mbagala lakini Serikali haikuridhia ombi hilo.
Akizungumza wakati wa kikao Cha pamoja kilichojumuisha Kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya ya Temeke, Baraza la Madiwani, Viongozi wa CCM Wilaya, RC Makalla amesema mchakato wa kuuza Eneo la Shule sio rahisi kwakuwa ni lazima Maombi yaanze ngazi ya Kata, Wilaya, Mkoa Kisha Mkoa upeleke Wizarani na Wizara iwasilishe ngazi ya juu.
Kutokana na hilo RC Makalla amesema amejiridhisha pasipokuwa na shaka kuwa eneo Hilo haliuzwi* na Halmashauri haina uwezo wa kufanya mauzo ya namna hiyo.
Aidha RC Makalla amesema Kikao hicho pia kimepitia taarifa ya Kamati iliyoundwa kupitia dosari zizojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa fedha za mikopo ya Asilimia 10 ya Halmashauri ya Temeke kwa Vikundi vya ujasiriamali ambapo ametangaza kuunda upya Kamati ya kufuatilia kwa kina suala Hilo ili itoe taarifa sahihi.
Kikao hicho pia kimejadili ajenda ya kufanikisha *Zoezi la anuani za Makazi na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 pamoja na mapokezi ya *Rais Samia Suluhu Hassan siku ya Jumapil ya Februari 20.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa