- Amesema utaratibu wa ugawaji utakuwa wa wazi, kipaumbele ni kwa wafanyabishara wa mwazo
-Atoa pongezi kwa NHC na mkandarasi kwa kasi ya Ujenzi huo
-Amshukuru Rais Dkt Samia kwa kuidhinisha pesa za Ujenzi wa Soko hilo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla leo Machi 9, 2023 ametembelea na kukagua maendeleo ya Ujenzi na Ukarabati wa Soko la karikaoo ambapo hadi kufikia sasa Ujenzi wa Soko jipya uko 65% na Ukarabati wa Soko la zamani uko 85%
CPA Makalla akiongea na vyombo vya habari Sokoni hapo ametoa rai kwa Wananchi kuepuka matapeli wanaowalaghai kuwa fremu za Soko hilo zimeanza kugawiwa ukweli ni kwamba fremu bado hazijagawiwa mradi ukikamilika utaratibu wa ugawaji utakuwa wazi kwa Wananchi wote.
Aidha CPA Makalla amempongeza msimamizi wa mradi ambaye ni Shirika la Nyumba la Taifa kwa usimamizi mzuri na mkandarasi anayejenga Soko hilo kutokana na kasi yake ambayo *inaleta matumaini ya kukamilisha Ujenzi kabla ya muda ulioko kwenye Mkataba.
Vilevile CPA Makalla amesema Soko limejengwa kisasa, tahadhari zote zimechukuliwa ikiwemo tahadhari dhidi ya majanga ya moto pia Soko litakuwa na uwezo wa kuchukua wafanyabishara wengi zaidi kuliko ilivyokua huko nyuma.
Mhe CPA Amos Makalla amemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha pesa nyingi za kukamilisha mradi huo, pesa zinakuja kwa wakati hakuna shida ya pesa ambapo amesema Soko litakapo kamilika wafanyabishara watafanya biashara masaa 24 mifumo ya Usalama itaimarishwa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa