Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla akiongea na wananchi wa Jimbo la Kinondoni katika viwanja vya Tandale Shule.
# Ataja Tandale ndipo atakapozindulia Kampeni ya Usafi
# Asema Billioni 150 zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Daraja na Mto Msimbazi
# Aunda Kamati Maalum ya Mazingira ya kuzuia Uharibifu wa Mazingira
# Asisitiza Ulinzi na Usalama
# Ampa OCD na Timu yake Wiki moja Kushughulikia KERO ya Uwanja wa Fisi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla leo tarehe 20 Septemba, 2021 ameendelea na ziara yake ya kupita Jimbo hadi Jimbo ambapo leo alikuwa Katika Jimbo la Kinondoni
Akiwa Kinondoni Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema Dar es Salaam inapaswa kuwa Safi katika kwani ameanza na Kuwapanga vema Wamachinga sasa anaenda Kuzindua Kampeni ya Usafi ambayo ataizindua katika Kata ya Tandale. "Wale wote walioanzisha magereji bubu yanayoweka magari barabarani waache Mara Moja". Alisisitiza RC Makalla
Wakati huo huo RC Makalla amesema kuwa Serikali imetenga kiasi cha Billioni 150 ili kujenga Mto Msimbazi ambapo Mto huo unaenda kukabiliwa mwanzoni aidha Mto Ng' ombe tayari mkandarasi yuko "site" na Kazi inaendelea
Kuhusu Kuunda Kamati Maalum ya Mazingira Mhe. Mkuu wa Mkoa amesema kuwa ameamua kufanya hivyo ili kuzuia waharibifu wa Mazingira na wachimbaji wa michanga ovyo katika Mito
Hata hivyo Mhe. Makalla amewataka wananchi wote kuendelea kudumisha Ulinzi na Usalama kwa maendeleo ya Taifa letu sambamba na kuwafichua wahalifu wote
Wakati huo huo Mhe. Mkuu wa Mkoa amempa muda wa Wiki moja OCD na Timu yake Kushughulikia KERO sugu ya Uwanja wa Fisi ili wananchi wakae kwa Amani na Utulivu
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa