RC Makalla akipima Urefu na Uzito kuashiria uzinduzi wa Kampeni ya Kupima Afya Bure katika Mkoa wa Dar es Salaam leo katika viwanja vya Tanganyika Packers.
RC Amos Makalla akipima presha mapema leo wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya Afya Check
- Wananchi wafurika Viwanja vya Tanganyika Packers kupima Afya
- Atoa ratiba ya zoezi la upimaji kila Wilaya.
- Awahimiza Wananchi kuchangamkia Fursa ya Upimaji.
- Zaidi ya Wananchi 15,000 kufikiwa na Zoezi hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Amos Makalla leo Juni 03 amezindua zoezi la Upimaji Afya Bure ambalo litafanyika kwa muda wa siku 10 ambapo Wakazi wa Mkoa huo watapata Fursa ya kupima magonjwa Bure Chini ya madaktari bingwa na wabobezi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers kwa Wilaya ya Kinondoni, RC Makalla amesema lengo la Kampeni ni kuwafikia zaidi ya Wananchi 15,000.
Aidha RC Makalla amesema kwa Wilaya ya Kinondoni zoezi litafanyika Leo na kesho Viwanja vya Tanganyika Packers Kisha kuhamia, Wilaya ya Temeke Juni 05 na 06 Viwanja vya Mwembeyanga*, Wilaya ya Kigamboni Juni 07 na 08 Viwanja vya Mjimwema, Wilaya ya Ubungo Juni 09 Hadi Juni 10 Viwanja vya Barafu na kuhitimishwa Wilaya ya Ilala Juni 11 mpaka Juni 12 Viwanja vya mnazi mmoja.
Hata hivyo RC Makalla amesema katika zoezi Hilo jopo la madaktari bingwa kutoka Hospital mbalimbali watahudumu zikiwemo Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Ocean Road, Taasisi ya mifupa MOI, Hospital ya Taifa Muhimbili, Agakhan, Chama Cha madaktari, Saifee, Hospital binafsi na Hospital za Halmashauri.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema miongoni mwa huduma zitakazotolewa ni upimaji magonjwa yasiyoambukizwa ikiwemo Kisukari, Shinikizo la Damu, Saratani na magonjwa mengineyo
RC Makalla amewashukuru na kuwapongeza Wadau waliofanikisha zoezi Hilo ikiwemo Clouds Media group Chini ya Mkurugenzi wake Joseph Kusaga, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Ocean Road, Hospital ya Taifa Muhimbili, MOI, AghaKhan, PCMC, TMH, Chama Cha madaktari, Red Cross, hospital za Manispaa, MDH, Tatu mzuka, Vodacom na wengieno.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa