- Afurahishwa na Ubunifu wa Benki ya NMB
-Asema NMB wamekuja wakati muafaka ambapo watanzania wengi bado hawana Akaunti
- Awataka wananchi kutumia fursa hiyo kufungua NMB PESA AKAUNTI
-Asisitiza NMB kutoa huduma hiyo nchi nzima
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo amezindua NMB pesa akounti hafla ambayo imefanyika katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Magufuli Mbezi-Ubungo Jijini Dar es Salaam.
RC Makalla akizindua huduma hiyo ya kidigitali amefurahishwa na ubunifu unaofanywa na NMB wa kuwawezesha wananchi kupata huduma mbalimbali za kifedha kwa kufungua akaunti popote walipo kwa gharama nafuu na haraka pamoja na kufanya miamala hapohapo kupitia simu ya kiganjani na gharama ya kufungua Akaunti hiyo ni kuanzia Tsh 1000 tu gharama ambayo wananchi wengi wanaweza.
Aidha RC Makalla amesema NMB wamekuja na huduma hiyo kwa muda muafaka ambapo wananchi wengi hawana akaunti hivyo amewataka wananchi kutumia fursa hiyo adhimu kufungua NMB Pesa Akaunti pia amesisitiza huduma hiyo itolewe nchi nzima* kwa kuwa inafaida kwa wananchi
Kwa Upende wa NMB wamesema huduma ni rahisi inafanyika kwa haraka pasipo mteja kujaza fomu kama ilivyozoeleka, mteja atafungua akaunti popote alipo na ataweza kufanya miamala papohapo bila kutumia kadi ni kupitia simu yoyote ile ya kiganjani na pesa atatoa kwa mawakala wa NMB walioko maeneo mbalimbali
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa