-Maelfu ya watu waungana nae kufanya usafi wa pamoja kuanzia fukwe ya Aghakan Kuelekea IFM na viunga vyake na kuhitimisha Viwanja vya Karimjee
-Wadau lukuki waunga Mkono Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DSM
- Atoa RAI Jamii kuendelea kuelimishana Juu ya USAFI kupitia mitandao ya Kijamii
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo amezindua Kampeni kabambe ya Usafi endelevu yenye kauli mbiu ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM
*RC Makalla* amezindua Kampeni hiyo kwa vitendo kwa kufanya usafi wa pamoja akianzia fukwe ya Aghakan, IFM na viunga vyake na kuhitimisha Viwanja vya Karimjee akiwa ameambatana na Viongozi wa Halmashauri ya Jiji la DSM, Viongozi wa Siasa, Wasanii ambao ni mabalozi wa Usafi na Watu wengine wengi.
Akiongea wakati wa kuhitimisha mbele ya waandishi wa habari amewashukuru watu wote waliojitokeza leo na kuungana naye katika kufanya usafi wa pamoja na *kuwataka kufanya usafi wa kila siku katika kaya lakini kila mwisho wa mwezi kufanya usafi wa pamoja
" Usafi wa pamoja ni Jumamosi ya mwisho wa mwezi mara moja kuanzia saa 12:00 hadi 3:00 Asubuhi ukimaliza mapema Ruksa kuendelea na majukumu mengine" Alisema RC Makalla
Aidha Mhe Makalla amepokea misaada mbalimbali ya vifaa vya usafi kutoka kwa wadau walijitokeza kuunga mkono Kampeni ambao ni NMB, GNM, Mabohora na Wengine wengi
Sambamba na hilo RC Makalla amewataka wananchi kutumia mitandao ya Kijamii Vizuri ikiwemo kuelimishana Juu ya Umuhimu wa Usafi na kuunga mkono juhudi ya Serikali ya Mkoa wa DSM katika Kampeni hii endelevu ya Usafi.
Mkuu wa Mkoa anaendelea kuwaomba wadau kuunga mkono Kampeni hiyo, Ofisi yake inamkaribisha yeyote atakaye kuwa tayari kusaidia katika Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM
USAFI UNAANZA NA WEWE " SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM" NDIO HABARI YA MJINI
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa