- Atoa maelekezo 8 kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Maafisa Elimu na Walimu.
- Awapongeza Walimu DSM kwa kutoa Elimu Bora na ufaulu mzuri.
- Awaahidi ushirikiano katika utatuzi wa changamoto zao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amezindua miongozo na mkakati wa Elimu ambapo amewaelekeza Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Maafisa Elimu kuhakikisha wanasimamia vizuri miongozo hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa majibu ya changamoto ili kuongeza ufaulu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo uliohusisha Walimu kutoka Shule mbalimbali za Mkoa huo, RC Makalla ametoa siku 14 kwa Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Maafisa Elimu kumpatia taarifa ya idadi ya Shule zenye migogoro ya Wananchi kuvamia na kujenga
Aidha RC Makalla ameelekeza kila Halmashauri kuanza maandalizi ya maoteo ya Wanafunzi kuanzia Shule za awali, Msingi na sekondari ili Ujenzi wa madarasa ufanyike mapema huku akisisitiza usimamizi madhubuti wa fedha na Miradi ya maendeleo.
Pamoja na hayo RC Makalla amewataka Maafisa Elimu kuhakikisha wanasimamia *Wanafunzi wa awali, darasa la kwanza Hadi la tatu wawe wanajua misingi nitatu ya elimu ambayo ni kusoma, kuandika na kuhesabu.
Ili kuhakikisha ubora wa Elimu na usikivu wa watoto, RC Makalla ametoa wito kwa Walimu kujenga hoja na ushawishi watoto wapate chakula mashuleni Baada ya tafiti nyingi kuonyesha ufaulu unategemea pia na Lishe Bora kwa Watoto.
Hata hivyo RC Makalla amesisitiza suala la mafunzo ya kuwajengea uwezo Walimu ili kuboresha kada hiyo huku akitaka Walimu kuthaminiwa na kuheshimika
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa