- Awataka wawe mfano wa kuigwa katika Jamii kwa kuwa wazalendo Na waadilifu.
- Wanaochaguliwa kujiunga JKT wajiunge pasipo visingizio.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka wahitimu wa mafunzo ya JKT kuwa sehemu ya kudhibi matukio ya uhalifu katika maeneo yao na kuwahimiza Wanaochaguliwa kujiunga na mafunzo hayo kujiunga pasipo visingizio.
RC Makalla amesema hayo Leo wakati akifunga rasmi Mafunzo ya Vijana wa Jeshi la kujenga Taifa JKT wa mujibu wa sheria kupitia Operesheni Jenerali Venance Mabeyo kwenye chuo Cha uongozi JKT Kimbiji ambapo amewataka wahitimu kuzingatia mafunzo waliyopatiwa.
Akizungumza na wahitimu hao RC Makalla amesema Mafunzo hayo ni muhimu kwakuwa yanawajenga vijana kuwa Wakakamavu, Wazalendo, Utii, Wawajibikaji na pia Elimu ya ujasiriamali.
Aidha RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi na Viongozi wa Serikali kuhakikisha wanaweka Mkazo kwa Watoto wao kupata mafunzo hayo ambapo miongoni mwa Vijana waliohitimu Leo ni pamoja na Mtoto wa Mkuu wa Mkoa.
Pamoja na hayo RC Makalla ametumia hafla hiyo kuwahakikishia Wakazi wa Dar es salaam kuwa Serikali kupitia Jeshi la polisi wamejidhatiti kuhakikisha wanadhibiti vijana wa Panya Road ambapo mpaka Sasa Jeshi Hilo linawashikilia vijana waliojihusisha na matukio hayo.
Hata hivyo RC Makalla amepongeza chuo Cha uongozi JKT Kimbiji kwa kuanza kutoa mafunzo hayo ambapo pia amezindua Kiwanda Cha kuzalisha mikate na vitafunwa ambacho kipo Chini ya Kambi hiyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa