- Ataka Jukwaa la wanawake DSM liwe la mfano ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan kufufua majukwaa ya wanawake nchi nzima.
- Asema wanawake ni jeshi kubwa, wasaidiwe Mafunzo ya ujasiriamali Na fedha
- Aelekeza Mamlaka za udhibiti ikiwemo TMDA, TBS na SIDO kuwatia moyo wazalishaji wazawa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam CPA, Amos Makalla ameelekeza Jukwaa la uwekezaji Wanawake kiuchumi Mkoa huo kuja na mpangokazi wa kuleta mabadiliko chanya kwa Wanawake ikiwa ni pamoja na kuwafikia wengi zaidi Ili kuleta tija na mabadiliko ya kiuchumi.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati ufunguzi wa Mafunzo maalumu kwa Viongozi wa majukwaa ya Wanawake Mkoani humo ambapo ameelekeza mafunzo waliyopata wakayashushe ngazi ya Wilaya, Kata na mitaa Ili kunufaisha Wanawake wengi zaidi.
Aidha CPA,Makalla ameelekeza dhana ya uwezeshaji Wanawake kiuchumi iende sambamba na kuwapatia fursa mbalimbali zinazopatikana Ili kuwakwamua kiuchumi.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan alilotoa kwa Kila Mkoa kuyalea na kuyatunza Majukwaa ya Wanawake.
Sanjari na hayo CPA, Makalla amewataka Viongozi wa majukwaa ya Wanawake kuelimisha Wanawake Kuhusu umuhimu wa kufanya mambo machache kwa ufanisi na tija na sio kujaribu Kila biashara
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa