-Asema wanapaswa kufanya ukarabati wa Vivuko vyao Mara kwa Mara kwa mujibu wa Kalenda
-Ataka Elimu ya N- Card iwe endelevu na ieleweke
- Atoa Rai wananchi kuzingatia Usafi wa Mazingira
-Awataka TEMESA kukarabati kivuko hicho Cha tatu kwa Umakini
- Kwa upande wa Meneja wa Vivuko Lokombe King'ombe akiri kupokea maelekezo hayo na kuyafanyia kazi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla ameendelea na ziara yake katika kutembelea Wilaya za Mkoa wa Dar es Salaam ili kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo ambapo Leo yupo katika Wilaya ya Kigamboni
Akiwa Katika Wilaya hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa ameanza na Daraja la Kigamboni ili kuona utendaji kazi wa Vivuko vya Kigamboni ambapo amewataka TEMESA kutokuweka Rehani Maisha ya Wanakigamboni kwani kwa Wanakigamboni *Kivuko ndio roho ya usafiri wao
RC Makalla amewataka TEMESA kufanya ukarabati wa Vivuko hivyo Mara kwa Mara kwa mujibu wa Kalenda kwani kila kivuko kinajulikana kinatakiwa kifanyiwe ukarabati kwa muda gani
Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka TEMESA kuendelea kutoa Elimu ya N- Card kwa wananchi ili waielewe sambamba na kuwasaidia wale wasiokuwa na Elimu hiyo pindi wanapokuja na pesa mkononi waweze kuvuka huku Elimu wakiendelea kupewa
Hata hivyo Mhe. Mkuu wa Mkoa amewataka TEMESA kukarabati kivuko hicho Cha tatu kwa Umakini Mkubwa ili kije kuwahudumia Wanakigamboni ipasavyo
Kwa upande wake Meneja wa Vivuko kanda ya Mashariki na Kusini Bw. lokombe King'ombe akiri kupokea maelekezo yote na kusema atayafanyia kazi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa