- Afunga Mafunzo ya siku 21 kwa wakufunzi wa Sensa ngazi ya Mkoa.
- Awataka kuzingatia kanuni na taratibu walizofundishwa.
- Awaonya wasijiingize kwenye mtego uliomkuta "NGOSWE" Kupitia hadithi ya NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE
- Sasa Elimu inahamia kwa Makarani na Wasimamizi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amehitimisha mafunzo ya Siku 21 kwa wakufunzi 1,064 wa Sensa ya watu na Makazi watakaokwenda kuwafundisha Makarani na Wasimamizi zaidi ya 10,000 wa zoezi Hilo linalotarajia kufanyika August 23.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo, RC Makalla ameelekeza wakufunzi hao kuhakikisha kile walichojifunza wanakifikisha kwa ufanisi mkubwa kwa Makarani na Wasimamizi wa zoezi la Sensa ili liwe na Tija.
Aidha RC Makalla amesema Mkoa huo umejipanga vizuri kuhakikisha Zoezi la Sensa linafanyika kwa ufanisi mkubwa Kama ilivyofanyika zoezi la Anuani za Makazi ambapo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya zoezi la Sensa kidigital
Ili kuhakikisha Elimu na hamasa ya Sensa inazidi kuwafikia watu wengi Zaidi, RC Makalla ameelekeza kila Wilaya kufanya Tamasha kubwa la burudani ambapo amesema Tamasha la Mkoa litafanyika kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers Kawe ambapo kutakuwa na burudani ya Mziki kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Kuhusu suala la ulinzi na usalama siku ya Sensa, RC Makalla amesema anataraji kufanya kikao kazi na Maafisa wa Vyombo vya usalama ili kuhakikisha Makarani na Wasimamizi wanafanya kazi yao pasipo usumbufu Wala uhalifu.
*#SENSA KWA MAENDELEO,JIANDAE KUHESABIWA#
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa