Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewaomba madiwani na Wenyeviti wa mtaa kushiriki kikamilifu katika kuhamasisha jamii katika Suala la usafi.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo katika kikao Cha madiwani na watendaji kata manispaa ya Temeke katika ziara yake ya kujitambulisha na kueleza vipaumbele kwa mkoa wa dar es salaam
ambapo amewaeleza madiwani na watendaji nanma ambavyo haridhishwi na Hali ya usafi Dar es salaam na kuwaomba kumuunga mkono kuiliweka jijii Safi.
Aidha RC Makalla ameeleza mpango wake wa kupendezesha mandhari ya mkoa, kuwapanga vizuri wamachinga na kuondosha magari mabovu yanayoharibu mandhari ya jiji hilo.
Katika kikao hicho RC Makalla pia amewapa vipaumbele vya kushughulikia ikiwemo Ulinzi na Usalama, Usimamizi miradi ya maendeleo, ukusanyaji wa Mapato, utatuzi wa kero za Wananchi na kuimarisha umoja na mshikamano.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa