RC Makalla akiwa na Wataalam wa Afya ambao ni Madaktari bingwa wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari kwa lengo la kutoa taarifa kwa Umma kuhusu Zoezi la Kupima afya bure Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Rashidi Mfaume akifafanua jambo wakati wa Mkutano huo na waandishi wa Habari
Muasisi wa Afya Check Dkt Isaack Maro akiongea mbele ya Waandishi wa Habari kuhusu zoezi la kupima Afya bure linalotarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 3/06/2022 katika viwanja vya Tanganyika Packers Kinondoni DSM
- Uzinduzi utafanyika Juni 3 viwanja Tanganyika Packers- Kawe
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema Mkoa huo kwa kushirikiana na Wadau wa Afya wanataraji kuanza zoezi la upimaji wa magonjwa mbalimbali Bure Afya Check kwa muda wa siku kumiambapo ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kupima Afya zao.
RC Makalla amesema ratiba ya zoezi Hilo itaanzia Wilaya ya Kinondoni Viwanja vya Tanganyika Packers Juni 03 mpaka Juni 04, Wilaya ya TemekeJuni 05 mpaka Juni 06 Viwanja vya Mwembeyanga, Wilaya ya Kigamboni Juni 07 Hadi Juni 08 Viwanja vya Mjimwema, Wilaya ya Ubungo Juni 09 Hadi Juni 10 Viwanja vya Barafu nna kuhitimishwa Wilaya ya Ilala Juni 11 mpaka Juni 12 Viwanja vya mnazi mmoja.
Aidha RC Makalla amesema Kampeni hiyo itaendeshwa na madaktari bingwa na wabobezi kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, Ocean Road, Taasisi ya mifupa MOI, Hospital ya Taifa Muhimbili, Agakhan, Chama Cha madaktari, Saifee, Hospital binafsi na Hospital za Halmashauri.
Hata hivyo RC Makalla katika siku kumi za upimaji Wananchi watapata Fursa ya kupima magonjwa mbalimbali yasiyoambukizwa ikiwemo Kisukari, Shinikizo la Damu, Saratani na magonjwa mengineyo, uchangiaji wa Damu na chanjo ya UVIKO19 ambapo amewahimiza Wananchi kujiwekea utaratibu wa kupima Afya Mara kwa Mara.
Pamoja na hayo RC Makalla amewashukuru Clouds Media group kupitia kipindi Cha Afya Check kinachoendeshwa na mtangazaji Dr.Isack Maro kwa kuamua kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kufanikisha Zoezi hilo.
Ili kufanikisha Zoezi hilo, RC Makalla ameelekeza Halmashauri zote za Mkoa huo kufanya maandalizi ya kutosha katika maeneo yao
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa