-Apongeza MDH kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa katika mambo mbalimbali ya Afya na hasa Mapambano ya Uviko-19
-Asema Wananchi wanahitaji kupatiwa maarifa na kuelimishwa Umuhimu wa Chanjo ya Uviko-19
-Asisitiza Mdau Mkubwa wa Afya yako ni wewe mwenyewe hivyo Ujanja ni Kuchanja
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla ameyasema hayo leo wakati anaongea na Wataalam wa Afya kutoka MDH na Sekretarieti ya Mkoa na Wilaya katika kikao cha kuweka mikakati ya Kampeni ya kuongeza kasi ya kuhamasisha Wananchi wa Mkoa wa DSM kuchanja chanjo ya Uviko-19.
Kikao hicho kilimefanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa JNCC Posta Ilala-Dar es Salaam.
RC Makalla amewapongeza MDH ( Management Development of Health) kwa kushirikiana na Serikali katika nyanja mbalimbali za Afya huku akibainisha MDH ni "partiner" mzuri wa Serikali.
"Ninauzoefu na NGO'S nyingi utakuta zina malengo mazuri na mikakati mingi lakini hakuna kinachofanyika niwapongeze sana MDH" Alisema RC Makalla
Aidha RC Makalla amesema wananchi katika makundi mbalimbali, popote walipo wahamasishwe na kupatiwa maarifa ya Umuhimu wa Chanjo ya Uviko-19 ili wawe na uelewa waweze kuchanja kwa hiari yao.
Hata hivyo RC Makalla amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa ya kupata chanjo na kuleta Chanjo za kutosha ambazo zimesaidia nchi yetu kuto kutengwa na kuwa sehemu ya Dunia kwa kuwa ilikuwa vigumu mtu kusafiri bila kuchanjwa.
Sambamba na hilo RC Makalla amebainisha *mdau namba moja wa Afya yako ni wewe mwenyewe hivyo Ujanja ni Kuchanja, Chanjo ya Uviko-19 ni Salaam imethibitishwa na Wataalam wa Afya
Kwa upande wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt Rashid Mfaume amesema hali ya uchanjaji kwa Mkoa sio mbaya sana kinachotakiwa ni kuendeleza kasi ya Uhamasishaji na uelimishaji wa jamii juu ya Umuhimu wa Chanjo ya Uviko-19.
Kikao hicho kiliwajumuisha Viongozi wa Amani (Dini) Mkoa wa DSM, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Wataalam kutoka MDH, Wilaya, na Sekretarieti ya Mkoa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa