.
RC Makalla akizima moto kwa kutumia kizima moto Anatoglo Mnazimmoja mara baada ya kumaliza kikao kazi cha mikakati ya mapambano dhidi ya majanga ya moto katika masoko
- Asema kila palipotokea Moto chanzo chake ni kujiunganishia umeme kiholela, kuacha maharage usiku na mateja kulala katika Masoko.
- Aagiza masoko yote yawe na fundi anayetambuliwa Na TANESCO.
- Aagiza Jeshi la Zimamoto kutoa Elimu ya kujikinga na majanga kwenye kila soko.
- Wakurugenzi Maafisa biashara waboreshe masoko, barabara, maji na kununua vizimia moto kila soko.
- Aagiza uongozi wa Masoko kuimarisha ulinzi wa Masoko.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo April 29 amefanya kikao Cha pamoja baina yake, Viongozi wa Masoko na Jeshi la Zimamoto na uokoaji kwa lengo la kutoa Elimu ya udhibiti wa Majanga ya Moto kwenye masoko ya Mkoa huo.
Uamuzi wa RC Makalla kuhitisha kikao hicho ni Kufuatia kuungua kwa baadhi ya Masoko ndani ya Muda ambapo ripoti za Kamati zinazoundwa kuchunguza zinaonyesha kuwa chanzo ni Uzembe wa watu kujiunganishia umeme kiholela na kinamama kuhinjika maharage kwenye majikoni usiku ili asubuhi wakute yameiva.
Kutokana na changamoto hiyo RC Makalla ameelekeza kila soko kuwa Vifaa vya kudhibiti moto na fundi wa umeme anaetambuliwa na TANESCO.
Aidha RC Makalla ameelekeza Jeshi la Zimamoto na uokoaji kuandaa ratiba ya kupita kila soko la Mkoa huo na kutoa Elimu ya kujikinga na majanga ya Moto.
Kuhusu changamoto ya uchakavu wa Masoko iliyolalamikiwa na Viongozi wa masoko, RC Makalla ameelekeza Kila Halmashauri kupitia Wakurugenzi na Maafisa biashara kuboresha Masoko, Barabara, Maji, Vyoo na kununua vizimia Moto.
Kwa upande wao Viongozi wa masoko Wamemshukuru RC Makalla kwa kuona tatizo lililopo na kuamua kuhitisha kikao Cha kupatia majibu changamoto ya Masoko kuuungua ambapo wameeleza kuwa kwa miaka mingi haijawahi kutokea kiongozi akahitisha kikao Kama hicho Cha kutoa Elimu ya kujikinga na majanga ya Moto hivyo kitendo alichofanya kimewapa matumaini makubwa.
Itakumbukwa kuwa hivi karibuni kumeibuka matukio ya kuungua moto kwa baadhi ya Masoko ikiwemo Soko la Kariakoo, Coca-cola, Karume, Mbagala na Soko la mchikichini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa