-Amshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kubariki ziara ya mafunzo kwa Viongozi wa makundi hayo nchini Rwanda
Atoa shukrani kwa NMB kuwezesha ticket za Viongozi 12 kwenda Rwanda
- Awataka kwenda kutengeneza mahusiano, kujifunza,na kupanua fursa za kibiashara
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam CPA Amos Makalla leo Februari 6, 2023 ameagana na Viongozi wa Machinga na Bodaboda katika Uwanja wa Mwl JK nyerere (JNIA) Terminal Three wakati wakipanda ndege kwenda Ziara ya mafunzo Nchini Rwanda
CPA Makalla wakati akiagana na Viongozi hao amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kubariki ziara hiyo ya mafunzo kwa Viongozi wamachinga na bodaboda kwenda nchini Rwanda
Aidha CPA Makalla amewashukuru Benki ya NMB kwa kufanikisha kuwapatia ticket za ndege 12 kwa mgawanyo wa Viongozi wa mchinga 5 bodaboda 5 na maafisa 2 wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo
Vilevile CPA Makalla amesema Rwanda imefakiwa kuwapanga wamachinga vizuri, udhibiti wa biashara holela pia bodaboda wanavituo vyao vizuri na wanafuata sheria hivyo Viongozi wa Machinga na Bodaboda watajifunza namna wenzao walivyofanikisha katika sekta hizo na kuwa *mabalozi wazuri pamoja na kutoa elimu kwa wenzao watakapo rudi Dar es Salaam
Sambamba na hilo CPA Makalla amewahakikishia tayari ameshaweka utaratibu mzuri wa Machinga na Bodaboda wa Rwanda kukutana na wa Dar es Salaam huku akiwataka kutumia fursa hiyo kujifunza,kutengeneza mahusiano ya namna bora wao kufanya biashara kwa masilahi mapana ya nchi hizi mbili.
Ifahamike kuwa ziara hiyo ya mafunzo nchini Rwanda ni ya siku 4 kuanzia leo Februari 6 ,2023 hadi Februari 10,2023
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa