- Ni Baada ya Mmiliki halali wa eneo Mzee Martin Nasson kukataa kulipwa fidia na Wavamizi.
- Viongozi wa Mtaa walioshiriki kuuza maeneo na kusababisha Mgogoro wakamatwa.
- Zaidi ya Shilingi Milioni 229 za Wananchi zimetafunwa na Viongozi hao.
- Wananchi WATAKIWA kuhama Na kuondosha maendelezo wenyewe.
- Awataka Wananchi kuacha tabia ya kuvamia maeneo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa muda wa siku 14 kwa Wananchi zaidi ya 700 wa Mtaa wa Mbondole Wilaya ya Ilala waliovamia na kujenga kwenye eneo la Mzee Martin Nasson kuondoka na kutoa wito kwa Wananchi kuacha tabia ya kuvamia maeneo.
RC Makalla ametangaza maamuzi hayo Baada ya Kukosekana kwa muafaka baina ya Mmiliki aliepewa haki na Mahakama kushindwa kukubali ombi la Wavamizi waliotaka kumlipa fidia ili waachwe kwenye eneo Hilo.
Kutona na Hilo RC Makalla amesema ifikapo Tarehe 18 mwezi huu asionekane mtu kwenye eneo Hilo na kusisitiza kuwa siku 14 zilizotolewa ni Huruma ya Serikali kwakuwa tayari walishaamuriwa na Mahakama kuondoka tokea muda mrefu.
Hata hivyo RC Makalla Serikali itaendelea kuheshimu Maamuzi yanayotolewa Muhimili wa Mahakama katika kusimamia Sheria.
Pamoja na hayo RC Makalla amewatahadharisha Wananchi kuacha tabia ya kuvamia au kununua maeneo pasipo kujiridhisha na Nyaraka za umiliki
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa