.
- Ataka usimamizi madhubuti wa Operesheni ya anuani za Makazi na Sensa.
- Aelekeza Agenda ya Ulinzi na usalama ipewe kipaombele kuanzia ngazi ya Mtaa.
- Asisitiza Udhibiti wa Biashara holela na Usafi.
- Watendaji wamuahidi kusimamia utekelezaji wa maelekezo hayo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla leo amefanya kikao kazi Cha maelekezo na Viongozi wa ngazi ya Wilaya, Kata na Mitaa wakiwemo Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa na Watendaji wa Kata/ Mitaa na kuwapatia maelekezo matano ya kutekeleza.
Miongoni mwa maelekezo hayo ni pamoja na Usimamizi madhubuti wa Operesheni ya anuani za Makazi ambapo amesema kwa Mkoa huo ni lazima zoezi Hilo lifanyike kwa ukubwa kwakuwa Dar es salaam ndio uso wa Nchi.
Aidha RC Makalla amewapongeza Viongozi na Wananchi kwa ushirikiano mkubwa walioonyesha kufanikisha awamu ya kwanza na kufanya Mkoa Kuvuka lengo kwa Asilimia 104 ambapo ameelekeza awamu hii ya pili ya uwekaji Nguzo kwenye Barabara, Mitaa na Vibao kwenye Nyumba kufanyika kwa Kasi na ufanisi.
Aidha RC Makalla amewataka Watendaji hao kuhakikisha Ifikapo August 23 kila Mwananchi anahesabiwa kwenye zoezi la Sensa ya watu na Makazi ili kuwezesha Serikali kujua idadi ya Wananchi na kuweza kupanga Bajeti na namna ya kutoa huduma.
Katika kikao kazi hicho, RC Makalla amewapongeza Wenyeviti wa Mitaa kwa kufanikisha Operesheni tokomeza Panya road jambo lililopelekea Jiji kuwa shwari ambapo ameelekeza agenda ya Ulinzi na usalama kuwa agenda ya kudumu kwenye vikao na mikutano.
Hata hivyo RC Makalla ameendelea kusisitiza Watendaji hao kudhibiti suala la Ufanyaji Biashara holela kwenye maeneo yaliyokatazwa ambapo amesema Mtendaji atakaeonekana kulegalega kwenye usimamizi atakuwa anapoteza sifa ya kuongoza eneo alilopo.
Kuhusu suala la Usafi RC Makalla ameelekeza Usimamizi wa Kampeni ya SAFISHA PENDEZESHA DAR ES SALAAM kwa kuhakikisha Wananchi wanafanya Usafi kila Jumamos na Usafi wa pamoja kila Jumamos ya mwisho wa Mwezi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa