- Asema wenyeviti wa mitaa ni watu muhimu sana katika kusukuma gurudumu la maendeleo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makalla leo Octoba 13, 2021 amekutana na Umoja wa wenyeviti wa mitaa Mkoa, Kigamboni Barakuda Beach - Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa amekutana na umoja wa wenyeviti wa mitaa akiwa kama mlezi wa wenyeviti Mkoa wa Dar es Salaam
Akiwa katika hafla hiyo alisomewa majina ya uongozi MPYA ambao unaongozwa na mwenyekiti mpya Mhe Juma Mwingamno Uongozi uliopatikana kutokana na uchaguzi uliofanyika.
Mhe Makalla amesema maendeleo katika Mkoa yanachangiwa na kazi kubwa inayofanywa na wenyeviti wa mitaa hivyo kupitia uongozi mpya uliopatikana ni vyema maelekezo yafuatayo yakazingatiwe na wenyeviti katika maeneo yao.
Kuhakikisha kila mtaa unakuwa Salama amewataka wenyeviti kusimamia usalama kwa kuwa na ulinzi shirikishi ili mitaa salama nyakati zote.
Kusimamia na kutatua Migogoro ya Ardhi Mhe Makalla amesema wenyeviti hao wasiwe sehemu ya Migogoro ya Ardhi, watunze maeneo ya wazi yasivamiwe na wananchi.
Usafi Mkuu wa Mkoa amesema Jiji la Dar es Salaam usafi hauridhishi amesema Novemba 6, 2021 atazindua rasmi kampeni ya usafi Mkoa wa Dar es Salaam awataka kusimamia zoezi hilo kikamilifu.
Kusimamia zoezi la kuwapanga Machinga Mhe Makalla amebainisha mbele ya wenyeviti hao biashara holela zinazofanyika zinachangia Jiji kuwa chafu hivyo wakasimamie zoezi hilo.
Miradi ya Maendeleo Mhe Mkuu wa Mkoa amesema Miradi yote inatekelezwa katika mitaa hivyo wenyeviti wa mitaa ni wadau muhimu katika Usimamizi wa Utekelezaji wa mradi mbalimbali katika maeneo yao.
Aidha Mhe Makalla amewataka wenyeviti wa mitaa kuwa mabalozi wa kuhamasisha Wananchi kuchanja chanjo ya Uviko -19 kwa kuwa ugonjwa huo upo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa wenyeviti mpya Mhe Juma Abas Mwangimno amemhakikishia Mkuu wa Mkoa utumishi uliotukuka. Vilevile Mkuu wa Mkoa amesema anazifahamu Changamoto zao yuko tayari kukaa kikao na yuko tayari kuwasemea.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa