- Asema Rais Samia ameelekeza Shirika kujiendesha kiuchumi na kibiashara Kama maono ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere
- Ataka Mali zote za DDC zilizoporwa/kuvamiwa kuainishwa ili zikombolewe.
- Aelekeza Bodi na Menejimenti kubadilika kifikra na kimtazamo Shirika lijiendeshe kibiashara
- Shirika liandae Mpango Mkakati wa Biashara wa muda mfupi, wa Kati na muda mrefu.
- Apongeza Maboresho yaliyoanza kufanyika Baada ya maelekezo aliyotoa
RC Makalla akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa Keko Millenium Lounge-Temeke
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameelekeza Shirika la Uchumi na Maendeleo la Jiji la Dar es salaam DDC kubainisha Mali zote zilizovaniwa au kuporwa ili aweze kuweka Nguvu kuhakikisha zinarejeshwa kwa mujibu wa sheria.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa DDC Millennium Lounge Keko Temeke ametaka Bodi na Menejimenti ya Shirika kubadilika kifikra na kimtazamo Shirika lijiendeshe kibiashara.
Aidha RC Makalla ameelekeza Shirika kuandaa Mpango Mkakati wa kibiashara kwa kutumia Vizuri rasilimali zinazomilikiwa na Shirika kukuza Uchumi.
Pamoja na hayo RC Makalla amesema Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuona DDC yenye mafanikio makubwa Kibiashara na kiuchumi kulingana na lengo la hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa