Mhe Amos Makalla akiwa studio za Clouds FM katika kipindi cha power breakfast mapema leo.
-Aelezea mkakati wake wa kuanza kusikiliza kero za wananchi katika majimbo ya pembezoni mwa Jiji, Agosti 30,2021 kuanza na Jimbo la Kawe
-Apongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kumdhibiti mualifu aliyesababisha vifo vya askari 3 na mgambo mmoja eneo la Sarenda bridge Jana Septemba 25, 2021
-Abainisha dhamira yake ya kuwaondoa wafanyabiashara holela ili kuliweka Jiji safi kwa kuweka utaratibu mzuri ambao hautaathiri biashara zao
-Azungumzia suala la kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo Dar es Salaam
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Amos Makala leo Agosti 26, 2021 amefanya ziara katika vituo viwili vya habari Wasafi na Clouds Media
Akiwa katika vituo hivyo alipata wasaa wa kutembezwa katika vyumba mbalimbali vinavyotumika katika uchakataji wa habari.
Mhe Makalla amevipongeza vituo hivyo kwa namna vinavyofanya kazi na kuahidi kufanya navyo kazi kwa kuwa tasnia ya habari ni mdau muhimu wa maendeleo.
Aidha Mkuu wa Mkoa amesema kuanzia Jumatatu ambayo ni Agosti 30, 2021 anaanza kusikiliza kero za wananchi katika majimbo ya pembezoni ambayo ni Kawe, Kibamba, Mbagala na Segerea akianza na Jimbo la Kawe eneo la Tanganyika Perkers huku akitoa rai kwa wananchi kujitokeza zoezi litaanza saa 2: 00 asubuhi na kutakuwa na timu wataalam wote
Mhe Makalla akizungumzia suala la usalama katika Mkoa amesema Mkoa uko salama wananchi waendelee kutekeleza majukumu yao ya kila siku, kwa upande wa tukio la jana amepongeza jeshi la Polisi kwa kumdhibiti mwalifu licha ya kuwa alifanikiwa kufanya mauaji ya watu 4 uchnguzi unaendelea ukikamilika ripoti itatolewa.
Sambamba na hilo Mhe Makalla amebainisha anavyo kwenda kukabiliana na wafanyabiashara holela pasipo kutumia nguvu, kwa sasa tayari mabango yanawekwa kuanisha maeneo ambayo hairusiwi kufanya biashara, ambapo kupitia zoezi hilo litasaidia kuufanya Mkoa kuwa safi.
Kwa upande wa miradi ya maendeleo amesema tayari ameshaelekeza kwa wakuu wa Wilaya katika Mkoa Salaam yake ni neno "MKUUU" tafsiri yake M- Mapato, K- Kero za wananchi, U- Ulinzi na Usalama, U- Usafi na U- Usimamizi wa miradi ya maendeleo,
"hivyo hizo herufi 5 lazima zisimamiwe vizuri kwa kila kiongozi na watumishi katika Mkoa wa Dar es Salaam" Alisema Mhe Makala
Mkuu wa Mkoa amesema amejipanga kuboresha fukwe zote ziwe kivutio cha utalii anaanza na Coco Beach pia yuko tayari kukutana chama cha wanamziki kuona namna bora ya kuboresha tasnia hiyo ya burudani.
Amesisitiza Wananchi kwenda kupata chanjo ya UVIKO-19 na kuendelea kuchukua tahadhari zote kwa kuwa ugonjwa huo upo.
Mhe Amos Makalla akiwa studio ya Wasafi FM katika kipindi cha Good Morning
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Anuani ya Posta: S.L.P. 5429
Simu ya mezani: +255 22 2203158
Simu ya mkononi: +255 22 2203156
Barua pepe: ras@dsm.go.tz
Haki Miliki © 2017 - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,haki zote zimehifadhiwa